RAIS wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh, JOHN MAGUFULI anatamani kumuona msanii wa muziki wa bongo fleva harmonize akigombea ubunge kwenye jimnbo analotoka la tandahimba.

  RAIS magufuli ametoa kauli hiyo oktoba 15, 2019 wakati akifanya mkutano wa hadhara mjini ruangwa mkoani lindi ambapo haromnize alitumbuiza kwenye mkutano huo.

   " nawapongeza sana waimbaji haya akina baba, lakini nampongeza sana harmonize ( Rajabu Abduli) sijui anatoka jimbo gani? amesema rais magufuli" Anatoka jimbo gani huyu tandahimba.Mbunge wa kule ni nani?" amehoji rais na kueleza "Aaaa, ningetamani kweli harmonize akagombea kule akawe mbunge wa tandahimba"

  kwa sasa jimbo la tandahimba linaongozwa na( CUF) Ahmad katani, hivyo huenda mwakani harmonize akatupa karata kugombea jimbo hilo kwa tikeyi ya ccm.

  Harmonize ni moja ya wasanii wa bongo fleva ambao wanafanya vizuri na akipewa nafasi ya kutumbuiza katika mikutano ya hadhara anayofanya rais.